HABARI ZA LEO MPENDWA MSOMAJI WA BLOGU HII !!
Pengine umewahi kuwaza Ni jinsi gani utakuwa msanii Bora hasa wa nyimbo za Hip Hop na umekosa majibu ya maswali yako.
Hii Ni Sehemu sahihi KABISA kwako,haujakosea kabisa kuingia katika blog hii itakayokusaidia kufanikiwa lengo lako kwa asilimia Mia moja.
Kwanza Tuanze na haya mambo ya Msingi ..
JE NAWEZAJE KUANDIKA MASHAIRI MAZURI YA WIMBO WA HIP-HOP ?
SWALI ZURI.....
Muziki wa hiphop Ni tofauti kidogo na aina nyingine za muziki Duniani.
UNAHITAJI maarifa mengi sana kichwani kabla ya kuamua kuanza KUANDIKA MASHAIRI yake.
UNAHITAJI
1.kuelewa mitaa
2.Kujua lugha ya mtaani
3.Kuwa na uwezo wa KUCHEZA NA maneno
4.kutumia mafumbo Na kadhalika.
Sio Jambo dogo kuandika wimbo Bora wa hiphop Kama hauna maarifa ya mambo Hayo hapo juu.
FUATA NJIA HIZI KUANDIKA WIMBO BORA WA HIPHOP.
1.MADA (CONTENT)
Hata mwalimu anapoingia darasani lazima awe na mada ya kufundisha, Wewe Ni mwalimu na wanafunzi Ni wasikilizaji wa kazi zako.
Je unawafundisha Nini?
Uhuni,ulevi,hekima,ujasiri,kutafuta fursa ? Au lolote lile.
Lazima uwe makini katika Hilo....
Zipo mada nzuri Sana za kuandikia wimbo na ukawa mzuri...
Mfano Kama MAPENZI,SIASA,MAISHA HALISI, UZALENDO N.K
2.MPANGILIO WA WIMBO WAKO.
kupangilia wimbo Ni Jambo Bora Sana la kuzingatia .
Miongoni mwa mipangilio mizuri ya nyimbo za hiphop Ni
Verse,chorus ,verse,chorus,bridge,chorus,outro.
3.Miondoko/Flow
Kamwe hautaandika wimbo Bora wa hiphop Kama hauna flow ya kuvutia.
Kauli inaweza kuwa Tata .
VUTA PICHA umevaa nguo mpya,nzuri na za kukupendeza lakini una Mwili mchafu .
Je Nini kitatokea?
JIBU unalo.
Unaweza ukawa na maandishi mazuri Sana lakini Kama flow yako Ni mbaya basi itachafua wimbo mzima.
Just work in your flow! Tumia midundo tofauti tofauti itakayofiti MASHAIRI yako katika muundo mzuri.
4.Tumia Mbinu za lugha ya kisanaa
Kama vile Methali,nahau na mafumbo katika uandishi wa kazi zako.
Msikilize mtu Kama Fid Q
Je unapenda mistari yake?
Hiyo Ni kwa sababu anatumia Mbinu za lugha ya kisanaa katika kazi zake.
SOMO LIJALO TUTAJIFUNZA AINA ZA MASHAIRI YA HIPHOP...
NA TUTACHAMBUA WASANII WAKALI WA HIPHOP TANZANIA.
COMMENT JINA LA MSANII UNAYEPENDA KUJUA UFUNDI WAKE HAPO CHINI ILI TULIFANYIE KAZI.
ASANTE.
0 Comments