Baada ya hapo twende sawa sasa.
Uandishi Kama Wa FID Q au Nikki M ishi?
Ngoja Tuanze na hao Kwanza.
JINSI YA KUANDIKA KAMA FARID KUBANDA AU "FID Q"
"Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo
sikuwa na umuhimu kihivyo stimu zikanipa elimu ya Biko
Kimaandiko kimistari.. hadi fans wanascream nikirap..
sikuamini kama nina zali mpaka nilipoidream hiphop"
Hayo Ni mashairi Yanayopatikana katika wimbo wake wa MAFANIKIO
Aliofanya na Baraka D Prince
Hapo Fid ametumia DOUBLE RHYMES AU VINA DABO.
Maneno Kama
ninaheshimu nilipo/elimu ya biko
wanascream nikirap/dream hiphop
Nadhani hapo umepata PICHA ya ninachomaanisha.
Katika uandishi huu ambao pia wanatumia wasanii wakubwa Duniani Kama Marehemu Big L, Rapper Fat Joe Na Jadakiss huwa unatakiwa utafute Kwanza vina vya mwisho kuliko maneno ya mwanzo.
Chukulia mfano unataka kurap KUHUSU Ugumu wa maisha.
Tafuta maneno kama
SHIDA /GIZA /MIDA/SHIBA/IBA
NYINGI/PIMBI / WIZI/CHIZI/SIMBI
HALAFU ANDIKA MSTARI KWA MFANO INAWEZA KUWA
"Mtaani hakuna kazi Ni SHIDA NYINGI..
Unaweza kuwa mwizi UKA-IBA SIMBI"
😁😁😁 Inasound POA?????
Hiyo Ni Mbinu ambayo ukiweza KUCHEZA nayo itakusaidia Sana katika uandishi wa Aina ya Fid Q.
Ushauri.
Sikiliza watu Kama P Mawenge,Nikki Mbishi, One,Srereo n.k Kama unataka kujua uandishi huu.
SOMO LIJALO TUTAANGALIA JINSI YA KUANDIKA STORYTELLING RAP SONG
COMMENT HAPO CHINI ILI NIJUE KUWA TUPO PAMOJA
💪💪💪💪
0 Comments